Habari Kitaifa

Waziri Mkuu MAJALIWA ashtukiza Bandari ya Dar es Salaam

on

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP. Simon Sirro kuwakamata Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark Bw. Samweli kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya semitela 44 bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo wakati alipofanya ziara ya ghafla bandarini baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kuutapeli uongozi wa TPA kutaka kutoa magari hayo yaliyoingizwa nchini mwaka 2015 kutoka nchini Uturuki, na kutaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu Serikali.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bw. Bahman wa kampuni ya NAS kutaka kupata msamaha wa kodi kwa kuidanganya TPA kwa madai kwamba wamewasiliana na Waziri Mkuu na wasipotekeleza jambo hilo watapata matatizo na Waziri Mkuu kusema kitendo cha kuyasajili magari hayo bila ya kuwa na nyaraka hizo ni kinyume cha sheria na pia kinaweza kusababisha kampuni iliyouza magari hayo ya Serin kutolipwa malipo yaliyobaki.

Amesema jambo hilo halikubaliki kwa sababu linaweza kudhohofisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Uturuki kwani tayari kampuni hiyo imeshawasilisha malalamiko hayo katika ofisi ya Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko alimueleza Waziri Mkuu kuwa pamoja na vitisho vya mfanyabiashara huyo kuwa wasipotekeleza matakwa yake watapata matatizo, lakini waliendelea kusimamia sheria na taratibu zilizopo bila ya kutetereka.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *