Uchumi Zone

Wanahabari Watakiwa Kushirikiana na Wizara ya Kilimo

on

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amewasihi  Wanahabari nchini  kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Kilimo ili ifanikiwe katika jitihada zake za kuhakikisha kwamba Tanzania inafikia azma yake ya Kuwa nchi ya Viwanda kwa kupitia sekta ya Kilimo ambayo imekuwa na Fursa kubwa katika Kuinua uchumi wa watu.
Hayo amezungumza katika Mkutano wake  wa wahariri pamoja na Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini ambao ulifanyika jijini Dar es Salaam wenye lengo la kujifunza  na kuongeza uelewa  juu ya Mifumo mipya iliyoanzishwa na Serikali kuhusu Uagizaji wa Mbolea kwa Pamoja  na Usimamizi wa bei Elekezi ya Mbolea nchini.
Mh Mwanjelwa alisema kuwa ipo Baja kwa Jamii kupata uwelewa mzuri kuhusu mifumo mipya ya Uaguzaji mbolea nchini  ili  Mkulima aweze kupata mbolea bora na kwa bei nafuu pamoja na kuongeza matumizi ya mbolea yatakayo chochea, ongezeko la uzalishaji wa chakula ambao utakidhi mahitaji ya familia na kujiongezea Kipato lakini bila msaada wa wanahabari wakulima hawataweza kuelewa vizuri.
“Wanahabari nyingi ndiyo nguzo yetu na tunahutaji tuwe na Masharikiano ya karibu ili kuweza kuinua sekta yetu ya kilimo hasa upande wa mbolea bado kuna Matatizo makubwa ya wauzaji kutofuata bei elekezi jambo ambalo linaumiza sana wakulima tunaomba mtusaidie kuelimisha Jamii kuhusiana na hilo” Alisema Mwanjelwa
Aliendelea kwa Kusema Kwamba serikali ina Mkakati wa kuongeza matumizi ya mbolea ambao umekuwa na umuhimu wa pekee hasa ikizingatiwa kwamba imeweka lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati unaoendeshwa kwa viwanda.
Alisema Kwa sehemu kubwa, viwanda hivyo vitategemea malighafi itokanayo na mazao ya kilimo. Hivyo ili, kufikia lengo hilo, lazima kila mmoja kutumia nafasi yake kuhakikisha kwamba tija itokanayo na Kilimo inaongezeka kwani Mbolea ni moja ya vichocheo vikubwa.
“Pamekuwepo na Mifumo mbalimbali iliyoanzishwa kwa lengo la kumsaidia  Mkulima kupata mbolea za kutosha ili aongeze tija na uzalishaji katika kilimo ambayo ni pamoja na ruzuku ya usafirishaji ili kuwezesha mbolea kuuzwa kwa bei moja nchi nzima (Pan Territorial Prices). Baadae ulifuata Mfumo wa wauzaji kulipwa sehemu ya bei na hivyo mbolea kuuzwa kwa bei chini kuliko bei ya Soko. Sambamba na Mfumo huo, kulikuwa na jitihada za kutengeneza mbolea hapa nchini ili kuepuka gharama kubwa za uagizaji” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Alisema taarifa zinabainisha kuwa Mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Mwanza na Geita wafanyabiashara hufungua mifuko na kuuza mbolea ya kupandia (DAP) kwa Tshs 2,000/= kwa kilo ili wapate Tshs 100,000/= kwa mfuko wa kilo 50 badala ya bei elekezi ya Tshs 51,000 – 56,000/=.
Aidha, Mbolea ya kukuzia (Urea) wanaiuza kwa Tshs 1,500/= kwa kilo ili wapate Tshs 75,000/= kwa mfuko wa kilo 50 badala ya bei elekezi ya Tshs 41,000 – 45,000/=. Pamoja na kuwauzia wakulima mbolea iliyopoteza ubora kwa kufunguliwa na kuachwa wazi, wafanyabiashara hawa wanawaingizia wakulima hasara kubwa ya mavuno.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *