Habari Kitaifa

Wajasiriamali Dar es Salaam wapatiwa Kiwanda cha Uzalishaji

on

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akiwa mgeni rasmi katika kuweka jiwe la msingi katika viwanda vidogo vidogo vya wajasiriamali (LODET CULTURE DESIGNER) eneo la Mwananyamala, ambapo ametoa wito kwa halmashauri kuwapa vipaumbele kinamama, vijana na walemavu.

Ujenzi huo umegharimu Shilingi millioni 99 ikijumuisha majengo matatu ikijumuisha vikundi sita vya wanawake, vijana na walemavu wanaojishughulisha na kutengeneza dawa za kusafisha chooni, sabuni za kuoga na kufua, batiki, mikate na viatu.

Mhe. Makonda ameziagiza Halmashauri zote kuiga mfano huo wa kujenga viwanda na kutoa asilimia 10 kwa makundi hayo ili kupunguza adha ya ajira kwa wananchi huku akiahidi kuwakutanisha vikundi 1000 vya wajasiriamali na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ili kuhakikisha wanatambulika rasmi na Serikali kuu.

“Serikali ina mpango wa kuzindua soko la wajasiriamali litakalofanyika kila mwezi viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa na lengo la kukuza na kutangaza bidhaa za ndani na kuendeleza uchumi wa Jiji na Nchi kiujumla” Aliongeza Makonda.

Kwa upande mwingine ameeleza kuwa Seikali pia imetenga milioni 997 kwaajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vya wajasiriamali na kuzitaka halamashauri zote kusimamia masoko na kuhakikisha miundombinu inakuwa mizuri na rafiki kwa wafanyabiashara.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndugu Spora Liana amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwaunga mkono kwenye jitihada zao na kuahidi wajasiriamali watapatiwa fursa kwenye Viwanda na masoko yaliyopo kwenye Jiji la Dar es Salaam.

About Filbert Yudatade

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *