Viwanjani

Timu ya Polisi Tanzania yapata shavu la pesa na jezi

on

Kampuni ya SportPesa imewapatia timu ya soka ya Polisi Tanzania vifaa vya michezo pamoja na fedha taslimu Shilingi Milioni 20.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo wakati wa makabidhiano hayo kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema wanatambua mchango mchango wa Jeshi la Polisi kwa jamii, kwa kuwa linafanya kaz kubwa kuhakikisha Nchi na wananchi wanakua salama.
“Tunatanguliza shukrani za dhati kwa SportPesa kwa vifaa hivi pamoja na fedha hizi na tuna waahidi hatutawaangusha, kwani timu yetu ilikuwa na uhaba wa vifaa mbalimbali na fedha mlizotupatia zitaisaidia timu kutatua shida mbalimbali” Alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro kwa niaba ya timu.
SportPesa ni Kampuni ya michezo ya kubashiri Nchini ambayo pia inazidhamini Klabu tatu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba, Yanga na Singida United.

About Filbert Yudatade

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *