Habari Kitaifa

Taarifa ya Tanesco Kuhusu Ubomoaji wa Jengo la Ofisi za Makao Makuu yake

on

Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unawafahamisha Wateja wake wote na Wananchi kwa ujumla kuwa; 

TANESCO  imeanza utekelezaji wa  Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli, kuhusu kubomolewa  kwa Jengo la Ofisi za TANESCO  Makao Makuu, liliopo Ubungo Jijini Dar es salam.  

Kuanzia Jumatatu Novemba 27, 2017 Ukuta wa mbele ya jengo umesha vunjwa ,  pia  baadhi ya Watumishi wa Shirika wameanza kuhamishiwa katika ofisi nyingine za  TANESCO zilizopo jijini Dar es salaam ili kupisha shughuli za ubomoaji kufanyika kwa usalama  zaidi. 

Uongozi wa Shirika   pamoja na Wakala wa Majengo (TBA) wanaendelea kufanya taratibu zitakazo wezesha zoezi la ubomoaji wa Jengo kufanyika bila kuathiri huduma kwa Wateja wa Shirika Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais.  

Tunapenda kuwahakikishia Wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Huduma za Umeme zitaendelea kupatikana kama kawaida ikiwemo huduma ya manunuzi ya LUKU.

Uongozi wa Shirika utaendelea kutoa taarifa kwa kadri zoezi hili linavyo endelea,     

Imetolewa Na:  OFISI YA UHUSIANO

                               TANESCO- MAKAO MAKUU.

                                Novemba 27, 2017

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *