Viwanjani

Simba SC na Azam FC zatoshana Nguvu, Chamazi Complex

on

Mechi ya Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara baina ya Azam FC na Simba SC imechezwa leo katika uwanja wa Azam Komplex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika hakuna timu iliyoona lango la timu nyingne.

Mchezo kati ya Timu hizo mbili kipindi cha kwanza ulikuwa na mashambulizi ya upande mmoja ambapo Azam FC kipindi cha kwanza wameshambuliwa sana huku wachezaji wa Simba SC John Bocco na Shiza Ramadhani wakikosa magoli ya wazi kwa nyakati tofauti huku wachezaji wa Azam FC Himid Mao na Salum Abubakar wakiambulia kadi za njano.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu lakini hakuna timu iliyoona lango la timu nyingine, huku wachezajki wa timu zoe mbili wakiambulia kadi za njano, kwa upande wa Simba James Koteii dakika ya 38, Salim Mbonde dakika ya 43, huku kwa upande wa Azam FC Bruce Kangwa dakika ya 27 na Stephen Kingue dakika ya 32 kipindi cha pili.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika Makocha wa timu zote mbili walizungumza na waandishi wa habari ambapo kwa upande wa kocha wa Azam Aristica Cioaba alisema mchezo ulikuwa mzuri timu zote zimecheza vizuri lakini mwamuzi hakuwa vizur kwenye maamuzi yake huku kwa upande wa kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja alisema timu yake ya Simba ilibidi ipate ponti zote tatu Azam Coplex lakini haikuwa hivyo wameshindwa kuchukua pointi tatu.

Nae Afisa habari wa Simba SC Haji Manara amewashukuru mashabiki waliofika kuishangilia timu yao, amewashukuru wachezaji kwa mchezo mzuri japokuwa hawakupata matokeo mazuri kwani nia yao ilikuwa ni ushindi na sio kutoka Sare ya bila kufungana na Azam FC.

“Tunawashukuru mashabiki. tunawashukuru wachezaji tumepata pointi moja, malengo yetu ilikuwa ni kuchukua pointi tatu mbele ya umati wa mashabiki waliokuja kutusapoti na mashabiki wengine, timu itakuwa na mapumziko kesho na jumatatu inaingia mazoezi kwaajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Mwadui FC” Alisema Manara.

Mechi katika uwanja wa Azam Complex imemalizika kwa timu hizo kupata sare tasa ya kutokufungana huku mchezo ukiwa mzuri bila kuwa na vurugu za aina yoyote, ulinzi kutoka Jeshi la Polisi ulikuwa wakutosha huku kukiwa na malalamiko machache kutoka kwa mashabiki kutokana na ufinyu wa uwanja hasa upande wa mashabiki.

Mchezaji wa Simba FC Erasto Nyoni akijaribu kumtoka beki wa Azam FC Aggrey Morris.

Haruna Niyonzima mchezaji wa Simba FC akitoa pasi kwa John Bocco (hayuko pichani) kwenye mechi ya Simba VS Azam Chamazi Complex.

About Filbert Yudatade

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *