Habari Kitaifa

Serikali yasaini Mkataba wa Ushirikiano katika Miradi ya Maendeleo ya Wanawake

on

Serikali imesaini Mkataba wa makubaliano wa Miradi ya Wanawake Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women).

 Akitia saini Mkataba huo kwa niaba ya Serikali Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga amesema kuwa Mkataba huo unahusu Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Wanawake Watanzania.

 Bi. Sihaba Nkinga ameongeza kuwa Mkataba huo  umeainisha maeneo ya ushirikiano ambayo ni  Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Kuondoa Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW),Kufanya Mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000,  Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/2021).

 Aidha Bi Sihaba Nkinga amesisitiza  kuwa Mkataba huo utasaidia kuendeleza jitihada za Serikali ya Tanzania na Wadau mbalimbali katika kufikia Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi.

 “ Makubaliano haya yatasaidia sana katika kusaidia juhudi za Serikali na Wadau  kumuwezesha wanawake wa Tanzania kujikwamua  kiuchumi na kufikia usawa wa kijinsia”alisema Bibi. Sihaba.

 Kwa upande wake Mwakilishi wa UN Women – Tanzania, Bibi Hodan Addou amesema kuwa pamoja na jitihada zilizofanyika kati ya Shirika hilo na Serikali katika kuwaletea Maendeleo Wanawake, jitihada zingine zitakazofanyika ni kusaidia juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania za kuongeza Ushiriki wa Wanawake katika Uongozi na kutoa maamuzi kwenye  ngazi zote. 

 “Tunaahidi kushirikiana naSerikali katika kumuinua na kumuendeleza mwanamke wa Kitanzania katika kujikwamua kiuchumi” alisema Bibi Hodan.

 Mkataba huo wa Mwaka mmoja (2017/2018) unalenga kumuwezesha mwanamke wa kitanzania kujiajiri, kujitegemea na hivyo kujikwamua kiuchumi kwa  kujiongezea kipato binafsi, familia na taifa kwa ujumla.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *