Habari Kitaifa

RC Makonda akabidhi Vitendea Kazi kwa Jeshi la Polisi, Dar es Salaam

on

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhi vitendea kazi kwa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ikiwa ni njia mojawapo ya kuliimarisha Jeshi hilo katika kupambana na uhalifu na matukio katika Jiji.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Chuo cha mafunzo ya Polisi Kurasini Jijini Jijini Dar es Salaam Mhe. Makonda amesema Jiji la Dar es Salaam limekuwa na muingiliano wa watu wengi wa aina mbalimbali hivyo inabidi Jeshi la Polisi Mkoa kuwa na mikakati ya kuweza kupambana na uhalifu wowote ule na yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ana wajibu wa kuhakikisha Mkoa wake unakuwa katika hali nzuri ikiwa ni pamoja na Usalama wa Raia wake.

“Nimejituma kufanya haya baada ya kuona Askari wangu wanafanya kazi katika mazingira magumu na pia Usalama wao upo katika hatari zaidi, maana Askari wangu wanauawa na kushambuliwa na majambazi kwahiyo mimi kama Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa baada ya matukio hayo kuniumiza sana hivyo nililazimika kutafuta njia ya kusaidia katika Jeshi na kuweza kupata ndugu zangu hawa kampuni ya TONGBA ambao leo wanatusaidia Pikipiki 10 ambazo ni kilometa sifuri pamoja na baiskeli 200 ambazo pia ni mpya kabisa ili ziweze kusaidia Jeshi la Polisi hapa Dar es Salaam” Alisema Mhe. Makonda.

Hata hivyo Mhe. Makonda alisisitiza Vitendea kazi hivyo vitumike katika kusaidia Jeshi hilo nasi kufanya mambo mengine tofauti na ilivyokusudiwa na kuahidi kutoa magari 56 yaliyokarabatiwa amabayo yalikuwa n mabovu na sasa yamekuwa yakisasa na yako katika hatua za mwisho za matengenezo ili yaweze kusaidia kukabiliana na uhalifu katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mbali na pikipiki hizo zilizotolewa na baiskeli mkuu huyo wa Mkoa alitoa na kompyuta za kisasa ambazo zitakuwa na mfumo wa kugundua kwa kuhifadhi taarifa kama mtu alishawai kufanya tukio Mbagala au kokote pale katika Mkoa huu na kuweza kuwa kesi hii ipo kwa Askari gani au Kamanda gani wa Wilaya.

Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam kamishina Msaidizi Wwandamizi wa Polisi Lazaro Mambosasa amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa msaada huo wa vifaa aliowakabidhi na kuahidi kuwa wao kama Jeshi la Polisi wanaahidi kutumia kwa waledi na sehemu husika na hakuna Askari yeyote atakayetumia vyombo hivyo kwa shuguli zake binafsi.

Pia kamanda Mambosasa alimuomba Mkuu wa Mkoa kutochoka kulisaidia jeshi hilo kwa vitendea kazi zaidi kwani wamekuwa na vitendea kazi ambavyo havitoshi kwa kuwa wana Askari wengi katika Mkoa huu hivyo aweze kuwasaidia kwa mra nyingine tena ili waendane na kasi yake ya utendaji.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwenye picha ya pamoja na ma                                            Kamishna wa Jeshi la Polisi Dar es Salaam.

     Makabidhiano ya Kompyuta kwaajili ya matumizi ya Kuhifadhi taarifa za                                                                        wahalifu kwa Jeshi hilo.

      Baiskeli zitakazotumiwa na Jeshi la Polisi Dar es Salaam kwaajili ya doria.

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akijaribu moja ya pikipiki 10 zilizotolewa na kampuni ya TONGBA kutoka China kwenye Viwanja vya Chuo cha Polisi Kurasini                                                                         Dar es Salaam.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akiwa ameongozana na            Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna Lazaro Mambosasa wakiwasili Chuo ch Mafunzo ya Polisi kurasini katika hafla ya kuwakabidhi Polisi                                                                                Vitendea kazi.

 

About Filbert Yudatade

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *