Habari Kitaifa

Mlinzi, Mfanyakazi Watajwa Katika Shambulizi la Meja Jenerali Mritaba

on

Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia Watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika katika tukio la kushambuliwa  kwa Meja Jenerali Mstaafu VINCENT MRITABA na watu wenye Silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni, Jijini Dar es salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, SACP LAZARO MAMBOSASA amemtaja mtuhumiwa wa awali kuwa ni Mlinzi aliyekuwa analinda nyumba yake ambae ni kutoka SUMA JKT.

Kamanda huyo ameeleza kuwa mtuhumiwa mwingine anaeshikiliwa na Jeshi hilo ni Mfanyakazi wa Benki ambayo Meja Jenerali Mstaafu VINCENT alienda kupata huduma.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kumkamata Jambazi aliyeongoza mashambulizi ya Askari 8 waliopoteza maisha huko Kibiti Mkoani Pwani.

Mbali na hilo Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam kwa mara nyingine tena limepiga marufuku biashara ya sialaha za jadi ambayo imeshamiri zaidi katika eneo la Ubungo, Jijini Dar es salaam.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *