Habari Kitaifa

Mawaziri wa SMZ na SMT watakiwa Kutekeleza Masuala ya Muungano Haraka

on

Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhesimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri wa Pande zote Mbili kutoka Tanzania bara na Visiwani Zanzibar kutekeleza Masuala ya Muungano kwa haraka na kwa Maslahi ya Pande zote mbili.
Maagizo hayo aliyatoa Mapema Jana katika Kikao na Mawaziri pamoja na Makatibu wao ambapo wataweza kujadili changamoto za Muungano zinazohusu Sekta ya Fedha,Uchukuzi na Biashara Kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
Akifungua Kikao hicho Makamu wa Rais Samia alisema kuwa kikao cha leo ni Maadalizi ya kikao kikubwa kijacho kitakachofanyika Mwanzoni mwa mwaka hapo Mwakani lakini katika vikao vya vilivyokaliwa na sekta zinagusa Muungano vilivyokaliwa hapo nyuma yapo Maazimio ambayo yalifikiwa kwenye vikao hivyo ila mengi bado hayajatekelezwa jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya nchi hasa upande wa Muungano.
Mheshimiwa Samia aliendelea kwa kusema kuwa hakuna haja ya manung’uniko pindi inapofikia makubaliano ya pamoja kwani kwa kufanya hivyo tunarudisha nyuma maendeleo katika Muungano.
“Jamani naomba sana Maamuzi ya Vikao vyetu tunavyokaa pande zote Mbili ya heshimike ili kuweza kuletea faida nchi yetu pamoja na kutimiza azma ya serikali yetu,Naona tunakaa na kufika Maamuzi lakini yapo mambo bado hayaendi ipasavyo sijajua mnakwama wapi huku Maamuzi kwenye vikao vyetu tushatoa”Alisema Mama Samia.
Aidha Makamu Mama Samia aliendela kwa kusema kwamba nbi kubwa ni kutunza Muungano wetu lakini kama kazi hazitafanyia ipasavyo ni kwamba tutavunja Muungano huu ambao umekuwa tunu kwetu.
“Si wakati wa kutunishiana Misuli tutambue kuwa pande hizi mbili tunategemeana sana katika Maslahi ya nchi hatuwezi kufikia Mafanikio kama hatataweza kufanya kazi ambazo sisi wenyewe tulikaa na kukubaliana ipo haja ya kila Pande kutambua umuhimu wa mwenzie ili kazi ziendelee ipasavyo”Aliendelea Samia.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira January Makamba alisema kuwa kinalenga Zaidi kupata Taarifa ya Kikao cha utekelezaji wa Maamuzi kwenye kikao lilicho kaliwa mwaka huu mwazoni pamoja na Vikao viwili vilivyokaliwa mwaka jana.
“Kikao hiki kimekuja baada ya Makamu wa Rais Kuitisha kikao hiki ili kuweza kupata ya masuala mabalimbali ya utekelezaji hasa katika Muungano ambapo Maamuzi kadhaa yaliwezakufikiwa awali na vikao vya nyuma lakini hakuna utekezaji ipasavyo”Alisema Makamba
Waziri Makmba alibainisha kuwa Kikao hicho kitakuwa na ajenda tatu za kujadili ambazo ni Kupata taarifa ya Utekelezaji wa Maamuzi kwenye Masuala ya Muungano kifedha,Taarifa ya utekelezaji wa Maamuzi ya serikali kusajili Vyombo vya Moto pamoja na Masuala ya Kibiashara.
Hata hivyo Kikao hicho kiliweza kuhudhuriwa na Mawaziri mbalimbali wa pande zote mbili,Makatibu wakuu pande zote pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *