Habari Kitaifa

LHRC: Uchaguzi mdogo wa Madiwani ulikuwa na Ukiukwaji mkubwa

on

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakisema Uchaguzi wa Madiwani wa kata 43 uliofanyika  jumapili nchi nzima uligubikwa na dhuruma, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeibuka na kusema wamebaini uvunjifu mkubwa wa haki za Binadamu  katika uchaguzi huo ambapo  CCM  walipata  ushindi wa kata 42 huku Chadema wakishinda  kata  1.

Akizungumza na   waandishi wa  habari leo Jijini Dar es Salaam  Kaimu Mkurugenzi wa LHRC Bi. Anna Henga wakati wakitoa tathmini ya Uchaguzi huo, amesema kituo hicho kimefuatilia kwa ukaribu uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani katika kata 43  zilizopo  halmashauri  takribani 36 kwenye mikao 19 nchini na kubaini uchaguzi ulikuwa na kasoro lukuki zilizochangia uvunjifu wa haki za binadamu.

“Vitendo hivi  vimefanywa  na Vyombo vya Dola,watu wasiojulikana na watu wanaosadikika kuwa wafuasi wa vyama siasa ikiwemo CCM na CHADEMA na vyama vingine vya upinzani na  matukio hayo ni pamoja na tukio la kukamatwa na kutekwa kwa watu  katika kata ya Kitwiru, Iringa mjini, kulikofanywa na vijana wa ulinzi wa CCM maarufu kwa jina la Green Gurd.” alisema Bi. Henga.

Aidha Bi. Henga amesema kuwa kituo hicho kimeitahadharisha Serikali kuwa kama isipokemea vitendo hivyo vya uvunjifu wa Haki za Binadamu kutasababisha athari  mbaya kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika 2019 pamoja na Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Bi. Henga aliongeza kuwa vitendo hivyo vimefanywa  na vyombo vya dola na watu wasiojulikana na watu wanaosadikika kuwa wafuasi wa vyama siasa ikiwemo CCM na CHADEMA na vyama vingine vya upinzani na  matukio hayo ni pamoja na tukio la kukamatwa na kutekwa kwa watu  katika kata ya Kitwiru iliyopo  Iringa mjini, kulikofanywa na vijana wa ulinzi wa CCM maarufu kwa jina la Green Gurd.

LHRC imebaini pia kuna matukio yameripotiwa kuhusu viongozi wa vyama vya viasa na mawakala wa vyama  kukamatwa mathalani Katibu wa Chadema Wilaya ya Ubungo ambaye alikuwa Mratibu Mkuu wa Uchaguzi wa Kata ya Saranga, Bw. Perfect Mwasiwelwa ambaye alikamatwa na Jeshi la Polisi.

Bi. Henga ameendelea kuyataja matukio hayo ni tukio la kukamatwa kwa Meya wa Ubungo na Mwenyekiti  wa Chadema Wilaya ya Ubungo Bw. Boniface Jacob ambaye alikamatwa siku ya uchaguzi ambaye ndiye aliekuwa aapishwe kuwa Wakala Mkuu kwenye majumuisho ya kura za  mwisho katika Kata.

 

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *