Uchumi Zone

Kampuni ya ZUKU FIBER yazindua huduma ya Internet yenye Kasi

on

Kampuni ya ZUKU FIBER, kampuni tanzu ya kundi la makampuni ya Wananchi leo imezindua huduma ya internet yenye kasi zaidi ya hadi 1oo Mbps kwa watumiaji wa mitandao Nchini Tanzania ikiwa lengo ni kutoa huduma ya internet yenye kasi zaidi kupitia vifaa vyake vya Triple Play.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la makampuni ya Wananchi Bw. Thomas Hintze, alisema uzinduzi wa mtandao wa internet yenye kasi zaidi Nchini Tanzania, Kifurushi cha ZUKU FIBER Triple Play 100 Mbps kimeundwa ili kukidhi mahitaji ya matumizi ya mtandaoni.

“Napenda kuwahamasisha wateja wanaotumia huduma za kisasa za mitandao kuijaribu ZUKU FIBER ili kuboresha uzoefu wao wa huduma hizo katika kuperuzi mambo mbalimbali mitandaoni ukiwa na kifaa chako kinachosapoti internet unapata kifurushi hiki cha Triple Play, Internet, Televisheni ya kidigitali na simu pia huduma hii ya mtandao tunatoa internet isiyo na kikomo” Alisema Bw. Hintze.

Naye Meneja wa Operesheni kutoka ZUKU FIBER Bw. Mcharo Mlaki aliongeza kuwa mbali na utoaji wa huduma ya Internet, kifurushi cha ZUKU Triple Play pia kinatoa huduma za Televisheni ikiwa ni pamoja na kuonyesha vituo maarufu vya Televisheni Nchini Tanzania na uteuzi mkubwa wa vituo vya Televisheni kama habari, michezo, sinema, Maisha na burudani.

Pia Bw. Mlaki alisema katika kusherekea uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi Nchini Tanzania wa ZUKU Fiber wateja wote watafurahia vifaa vya bure, ikiwemo moderm yenye uwezo wa wi-fi, Televisheni ya kidigitali zilizopo kwenye sanduku lenye thamani ya Tsh. 356,000 ikiwa ni bei punguzo, hivyo wateja wao wa ZUKU FIBER watahitaji tu kulipia ada ya malipo ya kila mwezi yenye gharama nafuu bila gharama zozote za ziada.

About Filbert Yudatade

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *