Habari Kitaifa

IGP SIRRO: azungumzia Wabaya wa Tundu Lissu

on

Ijumaa yenye tafakuri lukuki kwa kila Mtanzania, kutokana na wiki hii kutokea matukio kadhaa makubwa yaliyotikisa TAIFA  ikiwemo Kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki TUNDU LISSU, Kukamatwa  kwa kijana aliyeteka watoto mkoani  Arusha na vigogo kadhaa kutajwa katika ripoti ya Kamati ya Bunge iliyochunguza biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi .

Akionekana mtulivu na mwenye ari ya kuchapa kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP SIMON SIRRO anajitokeza mbele ya vyombo vya Habari na kusaidia kupunguza Tafakuri kwenye vichwa vya watanzania kuhusu suala la kupigwa risasi kwa TUNDU LISSU kwa kueleza hatua zilizochukuliwa hadi sasa na jeshi hilo..

Kwa mujibu wa jeshi la polisi ni kuwa hali ya usalama hapa nchini ni salama kwa kiasi cha kutosha licha ya matukio kadhaa ya kihalifu kutokea.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *