Habari Kitaifa

Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala Limeshindwa Kufanyika

on

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Charles Kuyeko ameahirisha kikao cha Baraza La Madiwani wa Manispaa hiyo kilichokuwuwa kifanyike leo kutokana na baadhi ya Wajumbe kutokuwepo katika kikao hicho.

Akizungumza na Madiwani na waandishi wa habari wakati anaahirisha kikao hicho Meya Charles Kuyeko ameeleza kuwa kikao hicho kilikuwa kiwe na Ajenda mbili ikiwemo ya kufanyika kwa uchaguzi wa Naibu Meya, ambaye kwa utaratibu uliopo Naibu Meya amemaliza muda wake, kutokana na sababu ya kutohudhuria Wajumbe hao ambao amesema walikuwa Ikulu kwaajili ya kushuhuia makabidhiano ya ripoti ya masuala ya madini.

“Naahirisha kikao hiki kutokana na baadhi ya Wajumbe kutokuwepo katika kikao hiki ambapo wapo Ikuu wanashuhudia makabidhiano yanayofanyika muda huu hivyo kikao kingine kitafanyika siku ya Jumanne tarehe 12 mwezi wa tisa mwaka huu saa nne kamili asubuhi” Alisema Meya Kuyeko.

Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala amabaye pia ni Msimamizi wa uchaguzi wa Manispaa hiyo alisema Mstahiki Meya wa Manispaa ameahirisha kikao hicho kutokana na idadi ya Wajumbe kutotimia kikanun, na hivyo kupelekea kikao kiahirishwe hadi siku hiyo ya Jumanne.

About Filbert Yudatade

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *