Habari Kitaifa

BancABC,Kitengo cha Dharura Muhimbili watoa Bima ya afya kwa watoto

on

BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imeshirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kutoa huduma ya bima ya afya itakayofaidisha watoto 100 ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia mradi mpya wa afya wa Muhimbili uliozinduliwa leo.

Akizindua mpango huo wa Afya wa Muhimbili Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, aliishukuru BancABC kwa kushirikiana na Hospitali ya Muhimbili katika suala hilo la kutoa huduma ya bima ya afya kwa watoto.

Alisema mradi huo wa Muhimbili kushirikiana na BancABC unaendea sambamba kabisa na malengo ya serikali iliyojiwekea katika kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma ya Afya kwa uhakika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani watoto ndio moja ya makundi ambayo huathirika sana wasipopatiwa huduma za Afya za uhakika.

“Natoa wito kwa wazazi watumie fursa hii iliyotolewa na BancABC kwa ushirikiano na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwafungulia watoto wao akaunti BancABC ili kuhakikisha watoto wao wanapata huduma kwa uhakika muda wowote bila ya ulazima wa kuwa na fedha tasilimu pale mtoto anapougua,” alisema.

Baadhi wa watoto wanufaika na kadi za bima wakiwa na walezi wao wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu.


Baadhi ya wafanyakazi wa Kitengo cha magonjwa ya dharura kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi 100 ambao ni Yatima.

Baadhi ya wafanyakazi BancABC Tanzania wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 ambao ni Yatima.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *